MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUKWA NA KATAVI KWA KUZINDUA KAMPENI YA SUMBAWANGA NG’ARA
Makamu
wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua Kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la
kudumisha usafi wa mazingira mjini Sumbawanga, wakati akimalizia ziara
yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha
Bilal na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya.
Mama
Asha Bilal, akionyesha mfano kwa kufagia wakati akimkabidhi mmoja wa
kinamama wanaofanya usafi wa mazingira katika mitaa ya mjini Sumbawanga,
jana wakati Makamu wa Rais alipokuwa akizindua kampeni ya Sumbawanga
Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa kampuni za kufanya
usafi katika mitaa ya mjini Sumbawanga, wakati akizindua kampeni ya
Sumbawanga Ng’ara kwa ajili ya kudumisha usafi wa mazingira, ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Mama Asha Bilal (kushoto kwake) na Mkuu
wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya (kulia kwake) na
baadhi ya viongozi wa mji wa Sumbawanga, mbele ya Sanamu la Sumbawanga
Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana.
No comments:
Post a Comment