Header Ads

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SOKO LA TUNDUMA LILILOUNGUA MOTO MWAKA JANA BAADA YA KUKARABATIWA UPYA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma jana, kwa ajili ya kuzindua soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto ulioteketeza soko hilo mwaka jana. Makamu wa Rais amewasili mkoani Mbeya jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Soko la Tunduma lililofanyiwa ukarabati baada ya kuungua moto mwaka jana, wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya jana.  Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa  Mbozi Magharibi David Silinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua Soko la Tunduma baada ya kukamilika kwa ukarabati kufuatia soko hilo kuungua motoa mwaka jana.

No comments:

Powered by Blogger.