Jumuiya ya Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA Watembelea Kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo

Mkurugenzi
Mkuu wa Maxmalipo Juma Rajabu akifafanua jambo kwa wakurungezi wa
serikali za mitaa kutoka Uganda , Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji Kanda
Group COO – Maxcom Africa Jamson Kassati , Kushoto Mwanzo Mr. Moses
Kimaro Kutoka ALAT (jumuiya ya serikali za MItaa Tanzania) na pembeni
yake katikati ni Mwenyekiti wa wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka
Uganda Dunstan Balaba ambapo Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za
Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo
Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii imeweza kugundua teknolojia
inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato
katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.
Mkuu wa
Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari Akifafanua
Jambo kwa Wakurugenzi hawa kutoka Uganda, Akielezea Jinsi mfumo wa
Ukusanyaji Kodi na tozo mbalimbali ulivyorahisisha upatikanaji wa mapato
katika halmashauri mbalimbali na Taasisi za Serikali kwa Ujumla na
kuzuia mianya ya upoteaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya
halmashauri.
Mwenyekiti
na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda Bwana Dunstan Balaba
Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza
Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo
Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo.
Wakurugenzi
wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA wakifuatilia Mada Kutoka kwa Mkuu wa
Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari
ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo Juma Rajabu anasema; Safari ya
kuuaminisha Umma na Serikali kwamba wazawa wanaweza kubuni mbinu
mbalimbali za kusaidia kuboresha makusanyo, inaenda sambamba na ufanisi
mzuri uliothibitika katika kazi mbalimbali ambazo kampuni Imekua
ikizifanya, Juma Rajabu ameongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo teknolojia
imerahisisha ulipajji wa bili mbalimbali Ikiwamo Luku, Kodi za TRA,
Ving’amuzi na hata ukusanyaji wa mapato kwenye vivuko.
Mmoja Wa
wakurugenzi kutoka Uganda Bibi Lilian Akiuliza Swali kwa Maxmalipo
wakati Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60
Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi
Gani kampuni hii Imeweza kuugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti
makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji
na majiji Nchini Tanzania.
Jumuiya
ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa mapema
leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani
kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo
kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji
Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment