TFDA YAKAMATA SHEHENA KUBWA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU DAR ES SALAAM
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya vipodozi
vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na
Serikali, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo akitowa maelekezo kwa maofisa wa (TFDA.
Mafundi wa (TFDA) wakiendelea na kazi.
Afisa
wa (TFDA) akiwa amebeba kiroba chenye vipodozi vyenye madhara kwa
watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es
Salaam.
Maofisa
wa (TFDA) wakipakia kwenye gari vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji
na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es
Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Jeshi la
Polisi, imefanyaukaguzi maalum na kufanikiwa kukamata shehena kubwa ya
vipodozi vilivyopigwa marufuku na Serikali katika baadhi ya majengo ya
Kariakoo jijini Dar es Salaam na thamani yake haijajulikana mara moja
haditathmini ikakapokamilika.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti B. Sillo
ambaye alikuwa nimiongoni mwa washiriki wa zoezi hilo kwa masikitiko
makubwa, alisema “ Kiasi cha vipodozi hivihatarishi vyenye madhara kwa
watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, ni kikubwakatika
historia ya ukaguzi hapa nchini na wafanyabiashara wote wanaohusika na
biashara hii haramu ni lazima wachukuliwe hatua stahiki za kisheria”.
Mkurugenzi
Mkuu huyo, aliendelea kusema kwamba kwa vile vipodozi hivi huingizwa
kwa njia yamagendo, ukaguzi huo ni endelevu na wahusika hawataweza
kukwepa mkono mrefu wa Serikali mahalipopote na wakati wowote.
Alitoa
rai kwa wafanyabiashara kuacha mara moja kuvunja Sheria za nchi na
wasalimishe kwa hiyari yao vipodozi vyote vilivyopigwa marufuku TFFDA
badala ya kusubiri Taasisi hiyo iwafuate.Katika hatuanyingine,
Mkurugenzi Mkuu huyo aliwaasa wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kutumia
vipodozisalama vilivyosajiliwa na Mamlaka na kuachana na vile
vilivyopigwa marufuku ili kulinda afya zao.Zoezihili limefanyika kuanzia
tarehe 21/4/2016 na haikuelezwa mara moja kwamba litaisha lini
No comments:
Post a Comment