MALINZI ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA INFATINO
RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma
salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini
Uswisi.
Katika
barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza
mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake
hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.

No comments:
Post a Comment