OLDUVAI GORGE IKO TANZANI SI KENYA
BODI
ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano
yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video
iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw
na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha
mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi
iko Tanzania kwamba iko Kenya.
Video
hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania
na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa
Olduvai Gorge iko Tanzania.
Bodi
ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza
vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji
mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi
nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine
katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.
Tunapenda
kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu
huyo wakati akihutubia mkutano amabao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa
Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. Tunapenda
dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo
binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey
waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka
takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine
popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa
katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani
Manyara nchini Tanzania.
Tunatoa
wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi
za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya
Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya
upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani
ya nchi au ya Kimataifa. Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania
kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB
kazi hii peke yake.
Yawezekana
katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata
fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia
walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea
ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
BODI YA UTALII TANZANIA.

No comments:
Post a Comment