FULL MKANDA PAMBANO LA CHEKA NA MSERBIA LEADERS JANA, CHEKA ASHINDA KWA ...'.POINTI'
Bondia
Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia
kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12
la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku
wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Katika
raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya
mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini,
jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na
kisha kuendelea na pambano.
Baada
ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana
kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake
akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa
na madhara kwa Cheka.Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi.
Cheka,
alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha
kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo
na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.
Cheka akitangazwa mshindi kwa pointi na mwamuzi kutoka chama cha ngumi WBF....
Cheka akishangilia ushindi wake.....
Mashabiki wakimbeba cheka kwa furaha.......
Cheka akivishwa mkanda wa ubingwa.....baada ya kutangazwa mshindi....
No comments:
Post a Comment