Leo ni Siku ya 'Rare Disease Duniani
Kila
mwaka Siku ya mwisho ya Mwezi Wa Pili huadhimishwa Siku ya 'Rare
Disease Duniani. Mwaka huu itakuwa leo tarehe 29 Feb 2016. Sharifa
Mbarak ni mama mwenye watoto wawili ambao waliathirika na magonjwa hayo
yasiyotambulika. Kesho ataongea na Waandishi wa habari na wadau
mbalimbali wakiwamo na madaktari wa watoto Dr. Mariam wa Agakhan na
Professor Kareem wa Muhimbili pamoja na Monica Joseph , mdau kutoka
Philips Medical Systems katika hotel ya Serena Dar es Salaam,Saa 4
asubuhi katika kampeni ya kuhamasisha magonjwa yasiyotambulika.
Tunaomba ushiriki wako katika siku hii muhimu kwa Watoto wa Sharifa na
watoto wote duniani wanaoteseka na magonjwa haya.

No comments:
Post a Comment