"TAASISI YA KANGA" YAZINDULIWA ZANZIBAR KUSAIDIA MAPAMBANO YA VIFO KWA WAJAWAZITO NA WATOTO
Baadhi
ya wageni waliohudhuria katika uzinduzi wa Taasisi ya KANGA ambayo
itahusika katika kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wadau kwa
lengo la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi wa
Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja
na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar. Picha
na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
Katibu
Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah
Talib kushoto na Mwenyekiti wa Taasisi ya KANGA Dkt.Mohamed Hafidh
kulia kwa pamoja wakiwakabidhi Viongozi kutoka Taasisi ya “DARAJA
Foundation” KEKI waliyoinunua katika harambee ya kuichangia Taasisi ya
Kanga kama njia ya kuiunga Mkono Taasisi hiyo. Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya KANGA Dkt.Mohamed Hafidh akitoa maelezo ya Taasisi hiyo
ambayo itahusika katika kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wadau
kwa lengo la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi
wa Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi
mmoja na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Katibu
Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah
Talib akitoa hutuba yake kabla ya kuizindua Taasisi ya KANGA ambayo
itahusikana ukusanyaji wa michango mbalimbali kutoka kwa wadau kwa lengo
la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi wa
Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja
na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar.
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 23/01/2016
Katika
kukabiliana na Vifo vya Wajawazito na Watoto Zanzibar Taasisi isiyo ya
kiserikali ijulikanayo kama KANGA imezinduliwa rasmi ikiwa ni mkakati wa
kukabiliana na tatizo hilo nchini.
Uzinduzi
wa Taasisi hiyo umefanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja
na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar.
Akitoa
ufafanuzi wa kuanzishwa kwake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Dkt.Mohamed
Hafidh amesema Serikali na Taasisi binafsi zinawajibu wa kuzidisha
mikakati ya kukabiliana na Vifo kwa akinamama na watoto ili kuwa na
taifa endelevu.
Amebainisha
kuwa wapo baadhi ya watu wenye uwezo wa kuchangia lakini wanashindwa
kujua wapi watapeleka Misaada yao ili kuokoa maisha ya watoto na
akinamama.
Dkt.
Mohamed ameongeza kuwa hata Serikali kupitia Wizara ya Afya inakabiliwa
na changamoto mbalimbali za matibabu nakwamba uwepo wa Taasisi ya KANGA
kutasaidia kwa kiasi kikubwa juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo
hilo nchini.
“Ukweli
nikwamba wapo wasamaria wema wanaguswa na hali ya vifo vya Wajawazito
na Watoto lakini wanashindwa wapi kwa kupeleka misaada yao lakini
kupitia Taasisi hii ya KANGA basi itakuwa ni sehemu muafaka ya kupeleka
misaada yao na bila shaka lengo litafikiwa”Alisema Dkt. Mohammed Hafidh
Dkt
Mohamed amesema hali ya Vifo nchini bado inatisha na kufafanua kwamba
kati ya Kinamama Wajawazito Laki moja,wastani wa 460 hupoteza maisha yao
nchini ambapo kwa nchi za Ulaya Idadi kama hiyo ni wastani wa watu sita
wanaopoteza maisha.
Ameongeza
kuwa Wastani wa Watoto 29 kati ya Elfu moja wanaozaliwa hufariki dunia
nchini Tanzania ambapo kwa nchi za Ulaya ni Wastani wa watoto watatu
wanaopoteza maisha miongoni mwa watoto Elfu moja.
Kwa
upande wake Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Katibu Mtendaji wa Kamisheni
ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah Talib amewaomba
Viongozi na wananchi kwa ujumla kuiunga mkono Taasisi hiyo kwa kuchangia
jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazowakabili wazazi na
Watoto katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
Amesema
kutokana na umuhimu wa jambo lenyewe ameahidi kukwata kiasi Fulani cha
Mshahara wake kila mwezi ili kuchangia harakati za Taasisi ya KANGA.
“Kwa
namna ambavyo nimeguswa na Malengo ya Taasisi ya KANGA na kwa namna
ambavyo Tatizo la Vifo kwa Wajawazito na watoto linavyoendelea naahidi
kukatwa Mshahara wangu kila mwezi kusapoti Taasisi hii”Alisema Shekh
Talib
Taasisi
ya KANGA ambayo imezinduliwa imejikita katika kujitolea kupambana na
tatizo la Vifo kwa watoto na akinamama wakati wa ujauzito ambapo pia
malengo ya baadae itaratibu uwepo wa Madaktari Wanawake wa kutosha ili
taratibu za Uzazi zote Hospitalini zifanywe na Wanawake wenyewe badala
ya Wanaume kama ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment