Zantel yatoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kukarabati shule ya Msingi Mkanyageni iliyoko Pemba.
Mkurugenzi
wa Biashara wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Bwana Mohamed Musa
akikabidhi hundi ya Shilingi millioni 10 kwa Mwenyekiti wa Shule ya
Msingi Mkanyageni, Bwana Ally Ngwali Vuai iliyoko visiwani Pemba kwa
ajili ya kukamiIsha ujenzi wa vyumba sita vya madarasa vitakavyotumiwa
na watoto zaidi ya 350. Anayeshuhudia ni Mkurugugenzi wa Mauzo Zantel,
Bwana Sukhwinder Bajwa pamoja na wanafunzi na wajumbe wa kamati ya shule hiyo.
Mkuu
wa Shule ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ramadhani Ngwali Makame, akitoa
neno la utangulizi wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni
10 baina ya shule hiyo na kampuni ya Zantel kanda ya Zanzibar.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo.
Zantel yatoa msaada wa shilingi milioni kumi kwa ajili ya kukarabati madarasa sita ya shule ya Msingi Mkanyageni iliyoko Pemba.
Pemba,Agosti 19,2015:Kampuni
ya simu za mkononi ya Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 10
kama mchango wa kujenga madarasa sita katika shule ya msingi ya
Mkanyageni iliyopo Pemba.
Kiasi
hicho cha fedha kitatumika katika kumalizia ujenzi wa madarasa hayo
sita kwa kuweka sakafu, madirisha na milango, kupaka rangi pamoja na
gharama za kazi kiujumla, msaada ambao unatarajiwa kuboresha kiwango cha
elimu katika shule hiyo.
Akikabidhi
msaada huo, Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni ya Zantel,Bw Sukhwinder
Bajwa alisema msaada huo umelenga kuboresha mazingira ya kusomea ya
wanafunzi wa shule hiyo.
‘Kampuni
ya Zantel mara zote imekuwa msitari wa mbele katika kuchangia kujenga
nchi kwa kushiriki katika kuwekeza katika shughuli za kijamii hasa
katika sekta ya elimu ambayo inaandaa mazingira na maisha bora ya
viongozi wajao katika upatikanaji wa elimu’ alisema Bwana Bajwa.
Akizungumza
pia wakati wa makabidhiano hayo, Mkurungezi wa Biashara wa Zantel
upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa alisema Zantel imejikita zaidi katika
kuhakikisha watoto wanapata elimu bora visiwani hapa.
‘Kama
kampuni inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja visiwani hapa ni wajibu
wetu kuhakikisha tunajitolea kwa kuwekeza katika miradi inayogusa maisha
ya wananchi kama huu wa elimu ambao unaboresha miundombinu ili watoto
wetu waweze kupata elimu bora’ alisema Mussa.
Akitoa
shukurani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada, Mwenyekiti wa kamati ya
shule, Bwana Ali Ngwali Vuai, alisema ni muhimu kuwekeza katika elimu
kwani wanafunzi wakielimishwa watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa letu.
No comments:
Post a Comment