ONGEZEKO LA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI TANZANIA 2015
Jovago Tanzania; Simu za kisasa zitumike
katika kukuza uchumi wa nchi
DAR ES SALAAM, 19 AUGUST, 2015; Matumizi ya
simu za kisasa (smartphones) yameonyesha kuongezeka kwa kasi ambapo zaidi ya Terabyte
76,000 hutumika kwa mwezi mmoja, hii imekuwa ni mara mbili ya takwimu
zilizofanyika mwaka 2013 ambapo kulikuwa na matumizi ya TB 37,500 kwa mwezi
mmoja katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara. (Ripoti ya Subsaharan Africa
Ericsson Mobility, 2014).
Kwa upande mwingine , soko la simu za kisasa
pia linakua kwa kasi, ambapo inaonyesha kuwa kutakuwa na ongezeko la mara mbili
ya manunuzi ya simu za kisasa (smartphones) katika miaka miwili ijayo, ambapo
Nokia, Samsung na Iphone ndizo zinanunuliwa kwa kasi katika miaka ya 2014/2015.
CNN
Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania anafafanua
kwamba, “Ongezeko la matumizi ya
smartphones hapa Tanzania linauwezo mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi hasa kupitia
biashara za mitandaoni, kutokana na muda mwingi wa watu wanautumia katika kuperuzi
kwenye simu zao”.
Guzzoni alifafanua kuwa, “kwa kadri miaka inavyozidi kuendelea, hakuna
mtu atakaye tafuta bidhaa au huduma yeyote bila ya kuanzia kwenye mtandao. Hii
ni kutokana na sababu za kuokoa muda na kukua kwa ulimwengu wa kidigitali na
utandawazi”.
“Faida au hasara
za simu za kisasa inatokana na matumizi yake, watu wengi wameelimika na wengine
hujipatia huduma bora kupitia mitandao, hivyo kuongezeka kwa matumizi ya
smartphones isiwe kwa ajili ya kuporomosha uchumi au maadili, bali iwe ni changamoto
katika kukuza uchumi wa nchi, mfano mzuri ni Nigeria ambao wako mbele katika
matumizi ya smartphones lakini sana wamekuza sekta ya utalii, kupitia Jovago.com”. Lilian
Kisasa, Meneja Mawasiliano wa JovagoTanzania.
“Iwapo
watumiaji wa simu za kisasa wanaendelea kuongezeka, hivyo hata wamiliki wa
biashara mbali mbali wanahitaji kubadili muelekeo wa biashara au huduma zao; “Japan
wanaendelea kukuza uchumi wao kwa kuuza zaidi ya 80% ya bidhaa zao kupitia
mitandaoni, hivyo hivyo na nchi zinazoendelea katika maendeleo ya kukuza uchumi
inabidi tukubaliane na hali halisi ya utandawazi kuwa masoko yanaingiliana na
wasitegemee aina moja ya kutoa huduma” alifafanua”.
Kwa Mwaka 2014, Tanzania imeshika nafasi ya 9
kwa nchi za kusini mwa bara la Africa, na nafasi ya 2 kati ya nchi za Africa ya
Mashariki kwa matumizi ya simu za mkononi, lakini pia inakadiliwa zaidi ya 25%
ya watu wanaotumia smartphones wanapata huduma zao za malazi, chakula, elimu,
na habari kupitia mitandaoni.
No comments:
Post a Comment