MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Ndugu Sabetha Mwambenja
mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius
Nyerere. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt.
Jakaya Kikwete tarehe 3.7.2015.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndugu Jacqueline Maleko
mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya
Sabasaba kwenye Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2015.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara wa TANTRADE, Ndugu Edwin Rutageruka wakati alipowasili kwenye
viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za
ufunguzi wa maonesho hayo uliofanya na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya
Kikwete tarehe 3.5.2015.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Anna Mkapa kutembelea
banda la Taasisi yake ya Fursa Sawa kwa wote (EOTF) mara baada ya
Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kufungua rasmi maonesho hayo tarehe
3.7.2015.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mwenyeji wake Mama Anna Mkapa
wakiangalia bidhaa mbalimbali za akina mama wajasiriamali kutoka mikoa
ya hapa nchini. Akina mama hao wanaratibiwa na Taasisi ya Fursa Sawa kwa
Wote inayoongozwa na Mama Anna Mkapa.

Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma
Kikwete akiwa na Mama Anna Mkapa wakifurahia bidhaa za vikapu
zilizotengenezwa na akina mama wajasiriamali kutoka mkoani Singida
kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya bidhaa mbalimbali za
asili wakati alipotembelea banda la Fursa Sawa Kwa Wote kwenye Maonesho
ya Sabasaba tarehe 3.7.2015. Kulia kwa Mama Salma ni Mama Anna Mkapa
akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema.
No comments:
Post a Comment