ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA SUMVE MKOANI MWANZA LEO.

Vijana 20 kutoka Sumve wakionyesha kadi zao za Chadema kabla ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema kutoka
kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520
walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve. Katika
ziara yake kwenye jimbo la Sumve Katibu Mkuu wa CCM amepokea kadi 48
kutoka Chadema ikiwa 28 zilizorudishwa katika kijiji cha Goloma kata ya
Mwadu.

kadi
za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya
zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika Sumve.

Wananchi
wa Kata ya malya wakionyesha Bango kubwa lenye ujumbe kwa Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana lenye madai ya kudhulumiwa viwanja
ambavyo tangia walipie miaka mitatu sasa hawajapata viwanja,Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungunza na wakazi wa kata ya
Malya ambao wanadai viwanja vyao walivyovilipia miaka mitatu
iliyopita,lakini mpaka sasa wananchi hao hajakabidhiwa,Ndugu Kinana
ameipa muda wa miezi miwili na ushehe kuwa ifikapo septemba 1,2015
,Halmashauri ya wilaya ya Sumve ihakikishe imelitatua tatizo hilo na
wananchi kupewa viwanja vyao. Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea
Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero
zao.


Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia sehemu ya kunyweshea
maji mifugo katika kijiji cha Kishilili, ambapo Ng'ombe zaidi ya 800
hupata huduma ya maji safi na salama katika mradi ambao pia husaidia
kaya 102 kupata maji safi na salama katika kisima kinachotumia mfumo wa
jua (solar power).

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya zege wakati
wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwashilalage.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nyambiti.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wakazi wa Sumve
wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano Sumve wilayani Kwimba.

Mbunge
wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndasa akiwasalimu wakazi wa Sumve
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Sumve
ambapo aliwahakikishia ahadi za CCM zitatekelezwa.

wakazi wa kata ya Sumve waliofika kwenye mkutano huo wa hadhara.
No comments:
Post a Comment