SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa zamani Mhe. Frederick Tluway Sumaye leo
ametangaza nia ya kugombea urais wa tanzania kwa mwaka wa 2015 kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza leo mbele ya wananchi na wanahabari katika Ukumbi wa
Hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Hoteli) jijini Dar es
Salaam, Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia ya kuwa mgombea urais
kutokana na alivyoweza kujipima mwenyewe, kujishauri na kutafuta ushauri
kutoka kwa watu wengine na kuona kweli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa amejitathimini na kuona kuwa yeye ndiye anayetosheleza
kuwa kiongozi wa nchi hii kutokana na jinsi alivyoweza kuongoza nchi hii
akiwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya miaka 9 na hivyo anastahili kuiongoza
nchi.
Aliongeza kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika
utumishi wa umma, kama ubunge, unaibu waziri, Uwaziri na hatimaye kuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania.
“Katika uongozi wangua nilijitahidi sana kusimamia uchumi wa taifa
kama vile, kusimamia uchumi, kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam iliyokuwa ikiongoza kwa uchafu wa mazingira miaka ya 1996,
kutengeneza madawati kwa shule zote za msingi, kuweka televisheni ya
taifa, mpango wa maendeleo Elimu (MMEM) na mambo mengine, ”alisema.
Vilevile alieleza juu ya kufanya kazi kwa muda huo wote katika ngazi
mbalimbali kuwa ni dhahiri nchi anaifahamu pamoja na shida za wananchi
pamoja na matatizo yao anayajua, kila eneo na kila kanda hivyo
akiteuliwa kuwa rais hatahitaji kujifunza juu ya nchi ya Tanzania.
Wakati akizidi kufafanua alieleza malengo yake endapo akiteuliwa kuwa
rais kuwa lazima atazingatia mambo yafuatayo ili kuweka uchumi imara
katika nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kulinda muungano pamoja
na amani na utulivu, kuimarisha uchumi, kupambana na maovu ya rushwa
kama vile ufisadi na madawa ya kulevya na mauaji, kuboresha huduma za
jamii na ajira pamoja na michezo.
Waziri Mkuu Mstaafu alipoulizwa swali juu ya ambao wote tayari
wamekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mwaka 2015 kuwa nani
anamwona kuwa kinara zaidi yake alisema kuwa yeye ndiye anafaa kuwa
kiongozi wa nchii hii kwani wote waliokwisha tangaza haoni kama wana
imani na kuongoza nchi yetu.
PICHA/STORI: DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment