OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA
Mkaguzi
Fahd Masanja (Katikati) akitoa elimu kuhusu Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa mmoja
wa wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kushoto ni Bw.
Roy Mchomvu, Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta wa Ofis ya Taifa ya Ukaguzi.
Bibi
Salma Pamui, Mkaguzi wa Idara ya Pensheni (aliyenyanyua mikono) akitoa elimu
kuhusu uhakiki wa taarifa za wastaafu kwa mwananchi aliyetembelea Banda la
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Idara ya Pensheni ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ni
Idara inayohakiki taarifa za wastaafu wote wa Serikali kabla ya kulipwa mafao yao.
Mkaguzi
Mariam
Chikwindo, mtaalam wa ukaguzi anayeshughulikia uhakiki wa matumizi
sahihi ya fedha za umma akitoa elimu juu ya uwazi katika matumizi ya
umma kwa wa wananchi waliotembelea
Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati wa Maonesho ya Wiki ya
Utumishi wa
Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es
Salaam.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Bi Sarah Reuben (Wapili kushoto)
akizungumza na mmoja wa wananchi waliojitokeza kujua kazi zinazofanywa na Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi. Wengine katika picha ni Wakaguzi, Bibi Tumaini Sorogo
(Kushoto) na Bw. Fahdi Masanja (Watatu kushoto).
Bibi
Tumaini Sorogo (Kushoto), Mkaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi akimsikiliza
kwa makini mwananchi aliyekuwa akiuliza taarifa mbalimbali kuhusu wajibu na
kazi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakati wa Maonesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015. Maonesho haya yanaendelea katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mchambuzi
wa Mifumo ya Kompyuta, Bw. Roy Mchomvu akimsikiliza kwa makini mwananchi
aliyetembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati wa Maonesho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkaguzi Salma Pamui (Kushoto) na Mkaguzi
Mariam Chikwindo (Wapili kulia).
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Bi Sarah Reuben (Kushoto) akizungumza
na mmoja wa wanahabari wakongwe nchini Tanzania, Bw. Pachal Mayala wakati wa Maonesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
Lenatus Leonard (Katikati) kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi akihojiwa kuhusu
ufanisi wa ukaguzi kwa upande wa Serikali za Mitaa na Bw. Pachal Mayala wakati
wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
PICHA
KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA TAIFA YA
UKAGUZI, MAKAO MAKUU








No comments:
Post a Comment