Mkurugenzi
wa Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Stephen Kilindo
(kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Kimarekani kwa
Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita,
Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga
na wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na
Mwanza. Fedha hizo zimetolewa na Kampuni SABMiller tanzu ya TBL.
Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu (kulia),
akifafanua jambo kuhusu msaada uliotolewa na Kampuni hiyo kwa ACE Afrika
kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga wa mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Wengine ni Meneja wa Fedha na Utawala wa
ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita (kushoto) na Mkurugenzi wa Sheria TBL,
Stephen Kilindo.
Meneja
wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita,
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea
mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa
mbogamboga katika mikoa ya Arusha,
Meneja
wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita,
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea
mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga
katika mikoa ya Arusha,
TBL YATOA MSAADA WA DOLA 24,000 TAASISI YA ACE AFRICA
Reviewed by
crispaseve
on
7:24 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment