ZIARA YA KATIBU WA CCM NDUGU KINANA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa
makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua
kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya
Kikwete kutoa fedha za mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada
ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano
wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe, utekelezaji
wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati
akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe
wilayani Mbongwe,mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwaga zege
katika zahanati ya kijiji cha Kasheko kata ya Lulembera wilayani Mbogwe
mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa wodi
ya akina mama inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Lugunga

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipaka rangi moja ya nyumba za
walimu zinazojengwa kwa nguvu za wananchi katika sekondari ya Mbogwe
kata ya Bwela.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lugunga,wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na Wana CCM katika katika kata ya
Mang'ombe kwenye kikao cha Halmashauri kuu Wilaya pamoja na kupokea
taarifa ya chama na serikali

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mganga Mkuu
wa kituo cha afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe,Dkt John
Mgosha,alipokagua kituo hicho na kuwasha umeme wa REA kituoni hapo,kulia
ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.Kinana na ujumbe wake
yupo katika ziara ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010-2015
inayotekelezwa na serikali.

Katibu
Mkuu wa CCM ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na kazi
zinazofanywa na vikundi vya wajasiliamali-Wanawake mjini Masumbwe
wilayani Mbogwe,Ndugu Kinana alikagua miradi mbalimbali ya vikundi hivyo
vya wajasiliamali.

Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa Masumbwe,wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia maelfu ya wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani
Mbogwe.
PICHA NA MICHUZI JR-MBOGWE, GEITA
No comments:
Post a Comment