MH.WAZIRI WA FEDHA SAADA M.SALUM AFANYA UKAGUZI WA ATUMIZI WA MASHINE ZA EFD KATIKA MADUKA MKOANI DODOMA.

Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum(MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA
mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart
kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara
bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.

Mh.Waziri
wa Fedha Saada M.Salum(MB) akimsikiliza msimamizi wa duka la Salome
Furniture wakati akijitetea baada ya kukutwa anafanya biashara bila ya
kutumia mashine ya EFD.

Waziri
wa Fedha Mh.Saada M.Salum(MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival
alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh.Waziri aliagiza
mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa
Mh.Waziri ni meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni
msimamizi wa mgahawa huo.

Waziri
wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum (MB) akiwa na Mh.Rukia Kassim Ahmed
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha wananchi CUF wakitoka kwenye
duka ambalo lilikutwa mmiliki wake akifanya biashara bila ya kutoa
risiti za mashine ya EFD. (Picha zote na Ramadhani Omary).

Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum (MB) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha
Bi.Ingiahedi Mduma mara baada ya kufanya ukaguzi wa matumizi ya mashine
za EFD katika duka mojawapo Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment