Header Ads

MHANDISI EDWIN NGONYANI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWENYE MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

????????????????????????????????????
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (kushoto) akisaini kitabu  cha wageni kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini.
????????????????????????????????????Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne  Shimba ( wa kwanza kulia) akimwonesha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (katikati)  moja ya  bidhaa zinazotengenezwa na  kituo hicho, kwenye  banda la Wizara ya Nishati na Madini
????????????????????????????????????Afisa Uhusiano kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Yisambi Shiwa (kulia) akieleza shughuli zinazofanywa na  wakala huo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (Kushoto) mara alipotembelea banda la wakala huo. Katikati ni Omari Rwakyaya kutoka wakala  huo.
????????????????????????????????????Kaimu Afisa Masoko Mkuu kutoka makao makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) (Katikati), Monica Massawe akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (Kushoto) mara alipotembelea banda la TANESCO. Kulia ni Afisa Uhusiano Wateja –TANESCO  Mkoa wa Illala, Lucas Kusare.
????????????????????????????????????Mtaalam kutoka Idara ya Nishati – Wizara  ya Nishati na Madini, Jacob Mayala (Kulia) akimweleza Abdul Naseka (Kushoto) majukumu  ya Idara ya Nishati kwenye maonesho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma  yanayoendelea katika  viwanja  vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

No comments:

Powered by Blogger.