MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MJINI BUKOBA LEO,AENDELEA KUJIZOLEA WADHAMINI


Umati
wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa
umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye
ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, leo Juni 15, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye
majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi
Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na
wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, Wakati akitoa
shukrani zake kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani
Kagera.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara
baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate
ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye
Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
No comments:
Post a Comment