KATIBU MKUU CCM NDUGU KINANA NA MSAFARA WAKE WAWASILI LEO MKOANI GEITA NA KUANZA ZIARA YA SIKU SITA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo.

Umati
wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya
Zamani.Katibu
Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inabidi ifute kodi
kandamizi zinazowazuia wananchi kurahisisha maisha yao.

Umati
wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya
Zamani.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo

Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana ukipokelewa katika kijiji cha
Kasenga,ukitokea mkoani Kagera,tayari kwa kuanza ziara ya siku 6 mkoani
Geita.

Ndugu Kinana akisalimiana na wananchi wa Kasenga,wilayani Chato mkoani Geita ikiwe ni sehemu ya mapokezi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi ofis mpya ya CCM katika kata ya Kasenga,wilaya ya Chato mkoani Geita.

Muonekano wa ofisi hiyo ya CCM

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi mara baada ya kuwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama
ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo,
wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita .
Kinana anaendelea na ziara
hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani
Kagera jana, Kinana anaendelea na ziara hiyo yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza
uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili
wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani kushoo na Katibu wa NEC itikadi na
Uenezi Nape Nnauye wakisoma bango lenye maanidishi lililobebwa na baadhi
ya vijana

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Paulina Sabinati mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.

Katibu
Mkuu wa CCM akizungumza na Wanachama wa Mshikamano Saccos wapatao zaidi
ya 400,ampapo pia alikabidhi mikopo kwa wanachama wa saccos hiyo
wapatao 20,kiasi cha shilingi milioni 78

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana pamoja na Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick
Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamoja na mafundi wa Tanesco
akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa umeme vijijini REA
katika kijiji cha Mkungo,wilayani Chato mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa
kijiji cha Makurugusi kuhusiana na mpango wa kupata umeme katika kijiji
chicho,ambapo kijiji chao kimerukwa na kuachwa bila kuweka umeme,hiuvyo
Wananchi hao wamemuomba Ndgugu Kinana kuhakikisha
anawasaidia na wao wanapata umeme katika kijiji chao.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akipeana tano na wananchi hao mara baada ya kuwaahidi
kuongea na Waziri wa Nishati na Madini ili kijiji hicho kiwekewe umeme
vijijini REA, ambapo wanakijiji hao walijawa na furaha mara baada ya
kusikia kauli hiyo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa CCM.

Umati
wa wananchi wa Chato mjini wakishangilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana aliyeanza ziara ya siku sita mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari katika
kijiji cha Ihanga wilayani Chato.

Wananchi wakinyanyua mikono yao juu juu kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia
wakazi wa Chato mjini ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chato ikiwa
siku yake ya kwanza ya ziara mkoani Geita baada ya kumaliza ziara ya
siku 10 mkoa wa Kagera.Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima
kukagua,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM
akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nnape Nnauye..

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani wa kata ya
Biziku Bw. Magomamoto Zanzibar akijinadi na kueleza namna alivyotekeleza
ilani ya uchaguzi ya CCM katika kata yake.
No comments:
Post a Comment