Header Ads

MAONYESHO YA TAASISI ZA KIFEDHA YA PESA EXPO KUFANYIKA MWEZI SEPTEMBA

1 (2)
Raymond Mhenge Mtaalam wa Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya PESAEXPO akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kebbys Mwenge jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kuhusu maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Sunday Mashele Mkurugenzi Mwenza Kampuni ya Exclusive Media na Godie Gervas Mkurugenzi wa Exclusive Media
1
Godie Mashelle Mkurugenzi wa Exclusive Media akisisitiza jambo katika mkutano huo kutoka kulia ni Eric Fussi Mkurugenzi Mwenza Qutub Grobal Limited na Sunday Mashele Mkurugenzi Mwenza Kampuni ya Exclusive Media.

Exclusive Media (T) Ltd ikishirikiana na Qutub Global Ltd imeandaa maonyesho makubwa yaTaasisi na asasi za kifedha nchini Tanzania yajulikanayo kama Pesa Expo.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa tisa jijini Dar es salaam.
Pesa Expo itahusisha Taasisi na asasi mbali mbali za kifedha Kama
  1. Mabenki
  2. Saccos
  3. Makampuni ya bima
  4. Makampuni yanayotoa huduma za Mikopo (Microfinance)
  5. Makampuni yanotoa huduma za fedha za kieletroniki
  6. Mifuko ya hifadhi ya jamii
  7. Makumpuni yanoyotoa huduma za kutuma fedha
  8. Soko la hisa na madalali wake
  9. Makampuni yanayotoa huduma za ushauri wa kifedha
  10. Taasisi zisizo za Faida zinazotoa Elimu kuhusu mambo ya fedha (NGOs)
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watanzania wana ufinyu wa elimu ya kutosha juu ya huduma nyingi za kifedha zitolewazo nchini pamoja na faida zake.Lengo kuu la Pesa Expo ni kuwakutanisha watoa huduma za kifedha pamoja na watumiaji wao na wananchi kwa ujumla.
Pesa Expo inapenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa asasi zote za kifedha nchini kushiriki maonyesho hayo.

Tayari baadhi ya makampuni yamesha thibitisha ushiriki wao hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wale ambao bado hawajathibitisha kuendelea kujitokeza na kuthibitisha ushiriki wao katika maonyesho haya Pesa Expo itatoa fursa mbali mbali kwa makampuni shiriki kama vile
Kufanya mauzo ya moja kwa moja Kutangaza huduma zao mpya Kutoa elimu ya huduma za kwa wananchi Kuboresha mahusiano yao na wateja Kuboresha mahusiano baina ya makampuni shiriki Kubadilishana mawazo na wajasiriamali na wananchi
Kufanya tafiti ya bidhaa zao Kujitangaza nk

Pesa Expo ni maonyesho endelevu yatakayokuwa likifanyika kila mwaka likianzia Dar es salaam na kuzuunguka mikoa mbali mbali nchini. Kwa hiyo tunawakaribisha Taasisi na asasi zote za kifedha na wadau wote wa masuala ya fedha nchini na wananchi kwa ujumla kuweza kushirikiana nasi kuweza kufanikisha maonyesho haya

No comments:

Powered by Blogger.