KAMISHNA WA MADINI AZITAKA TAASISI ZA MAZINGIRA NCHINI KUONGEZA USHIRIKIANO KWENYE MIGODI

Mijiolojia
wa Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe akizungumzia sekta ya
madini nchini kabla ya kumkaribisha Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa
Migodi, Mhandisi Ally Samaje ili aweze kufungua mafunzo kwa wataalam wa
Wizara. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi
za Madini Nchini na kufanyika Bagamoyo mkoani Pwani, yanatolewa na
Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka India, lengo likiwa ni
kubadilishana uzoefu na kuwapa uelewa katika usimamizi wa mazingira
kwenye migodi.

Kamishna
Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya
Nishati na Madini akifungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna
Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini yanayoendelea mjini Bagamoyo
mkoani Pwani.

Kamishna
Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya
Nishati na Madini (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele) pamoja na
washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na
wataalam kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India
(hawapo pichani) katika mafunzo kuhusu usimamizi wa mazingira migodini
yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Sehemu
ya wataalam kutoka Idara ya Madini iliyopo chini ya Wizara ya Nishati
na Madini wakifuatilia kwa makini mada kuhusu usimamizi wa mazingira
kwenye migodi katika nchi ya India iliyokuwa inawasilishwa na mtaalam
mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit
Kumar Singh (hayupo pichani) kwenye mafunzo hayo.

Mtaalam kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.

Mtaalam
mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India,
Sujit Kumar Singh akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.

Kamishna
Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya
Nishati na Madini (wa tatu kutoka kushoto, waliokaa mbele), Mkuu wa
Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi
Gideon Kasege ( wa pili kutoka kulia, waliokaa mbele) wakiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment