MABOMU YATAWALA CHUO CHA KAMPALA
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kimataifa Cha Kampala (KIU) leo wameandamana na katika chuo hicho
kushinikiza warudishe fedha zao kutokana na kuanzisha kitivo ambacho
hakitambuliki na mamlaka za nchi.
Mgomo huo umeanza majira ya saa
tatu kwa baadhi wanafunzi kuwazuia wenzao wasiingie katika chumba cha
mtihani na baada ya hapo wakaibuka na mabango kwenda katika ofisi za
utawala wa chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
katika chuo hicho,Rais wa Serikali wa Chuo Kikuu cha
Kampala(Kiupeso),Elias Mbogho amesema kuwa maandamano hayo yametokana na
baadhi ya wanafunzi waliohitimu ngazi ya cheti ya ufamasia kudai leseni
na kuambiwa chuo hakitambuliki ndipo chanzo kiliazia hapo.
Mbogho
amesema kuwa hatua mbalimbali zilishapita na kujiridhisha kuwa
kinatambulika lakini wanafunzi wakitivo hicho wameendelea kuweka
malumbano.
Afisa uhusiano wa chuo hicho ,Keneth Uki amesema kuwa
mgogoro huo ulishapewa suluhu kwa kupitia hatua za mamlaka za serikali
na kudhibitisha kutambuliwa chuo hicho.
Askari
wa Polisi wakiwa katika gari na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kampala (KIU) waliowakamata katika maandamano hayo.
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIUPESO),Elias
Mbogho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maandamano yaliyofanyika leo katika hicho jijini Dar es Salaam,Kushoto
ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi,Jamal Mohamed.
Wanafunzi wa KIU wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa kazini leo katika Chuo Kikuu cha Kampala jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala akiwa na majeraha katika maandano yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa katika maandamano katika Chuo Kikuu cha Kampala leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.
No comments:
Post a Comment