MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA NCHINI

Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa
bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei
kwa mwezi Mei,2015 umefikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5
iliyokuwepo mwezi Aprili, 2015.

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo leo.
…………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei
2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5 ya mwezi
Aprili 2015 kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei ya
bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei nchini
kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula
zinazotumiwa kwa wingi na kaya binafsi kwa mwezi Mei.
Amesema
bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka
kwa mfumuko huo ni Nyama,Choroko, Maharage,samaki, nyama,unga wa
mihogo.
Kwa
upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko
wa bei ni bei za mavazi ya wananume kwa asilimia 5.6, mavazi ya
wanawake kwa asilimia 3.5, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 4.1 na
huduma za malazi kwa asilimia 4.2.
No comments:
Post a Comment