KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE BUKOBA VIJIJINI,KESHO KUUNGURUA WILAYA YA MISENYI MKOANI KAGERA.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa katika uwanja wa
Katoro,kwenye mkutano wa hadhara Bukoba vijijini mkoani Kagera jioni ya
leo.

Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na
kuwaleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la
kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba
mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro
Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella.

Mbunge
wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh Jason Rweikiza akiwahutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Katoro Bukoba
Vijijini.

Wananchi
wa Katoro wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika mkutano
wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini mkoani
Kagera.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi wa kijiji
cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini,mkoani Kagera.

Wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Katoro wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera jioni ya leo

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera.


Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye Kikao cha kupokea
taarifa ya chama na serikali na kuzungumza na halmashauri kuu ya
Wilaya,kabla ya kuendelea na ziara yake katika wilaya ya Bukoba Vijijini
leo. Kinana amewataka viongozi wote kutokuwa na wagombea wao mioyoni
katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pia amewataka
wapambe wa viongozi kuacha umbea wa kuuza maneno kutoka huku kwenda kule
kwa sababu hali hiyo ni chanzo cha fitina miongoni mwa viongozi na
wanachama.

Baadhi ya Wananchi wa Kemondo wakishangilia jambo

Wananchi wa Kemondo wakifuatilia yaliyokuwa yakijri kwenye mkutano wa hadhara,Bukoba vijijini mkoani Kagera.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo,Bukoba Vijijini mkoani
Kagera .

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo, akiwa katika ziara ya
kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya ya
Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.

Wananchi
wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Ujumbe wake
walipokuwa wakiwasili katika kijiji cha Rukoma,Bukoba vijijini mkoani
Kagera.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji
cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya Ofisi ya CCM ya Kijiji
cha Rukoma aliyoindua leo, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani
Kagera,kulai ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni
Mbunge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza
No comments:
Post a Comment