Header Ads

CHAMA CHA ACT CHATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI EDSON KAMUKARA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
……………………………………………………
CHAMA cha Alliance ForChange and Transparance( ACT- Wazalendo.)kinachozingatia msingi wa utu, undugu na uzalendo kwa Taifa,kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwandishi wa Habari Edson Kamukara.
Kutokana na msiba huo Chama kinatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, ndugu jamaa na marafiki,waaandishi wa Habari na wafanyakazi wote wa Hali Halisi Publishers kwa kuondokewa na mtu ambaye mchango wake kwa Taifa ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu katika nchi
Tunawaombea kwa mungu wawe na uvumilivu na kuzidi kumuombea marehemu apate pumziko la amani.
Kichama tumempoteza mtu aliyekuwa akituelekeza upungufu wetu kupitia kalamu yake hali iliyotufanya tujirekebishe kila tunapobaini ukweli wa ukosoaji wake.
Tunazidi kumuombea kwa Mungu ampe faraja katika utangulizi wake huu, huku tukiwa na mengi mema ya kujifunza kutoka kwake.
Imetolewa na
Samson Mwigamba
Katibu Mkuu Taifa ACT-Wazalendo
Juni 26,2015

No comments:

Powered by Blogger.