BOT YAWATAHADHARISHA WANANCHI
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi
Mduma, akimpatia vipeperushi Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Zalia Mbeo, wakati alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya Wiki ya Utumishi, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi
Mduma, akimpatia vipeperushi Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Zalia Mbeo, wakati alipotembelea banda la wizara katika maonesho
ya Wiki ya Utumishi, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia maelezo Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB
Mkwizu, kuhusu kazi ya Benki Kuu, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
Meneja
Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia
maelezo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, HAB Mkwizu, kuhusu sarafu ya sh. 500, wakati wa ufunguzi wa
maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es
Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zalia Mbeo, akimpatia maelezo Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB
Mkwizu, kuhusu sarafu ya sh. 500, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
(Picha zote na Kassim Mbarouk)
Na Salma Ngwilizi – Maelezo
BENKI ya
Tanzania(BOT) imewataadharisha wananchi kwamba sarafu ya sh. 500
haina madini ya aina yoyote na wala haiuzwi haiuzwi kama inavyoadaiwa
na baadhi ya watu.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Zalia Mbeo
wakati akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mwizu ambaye aliuliza
kwamba kuna taarifa kuhusu sarafu hiyo kuuzwa mitaani.
Kaimu
Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma,
kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Mhe. Celina Kombani.
“Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.
Aliongeza
wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini
ambayo yanaweza kuwapatia fedha nyingi wakati si kweli.
Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa rasmi jana Juni 16, mwaka huu na yanatarajia kumalizika Juni 23, mwaka huu.
Kauli
mbiu ya mwaka huu “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya
kuwawezesha Wanawake kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa
Umma”.
No comments:
Post a Comment