ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA WILAYA YA BUKOMBE MKOAN GEITA.

Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukivuka mto kuelekea
katika kijiji cha Ilyanchele wilayani Bukombe wakati akiwa katika ziara
ya kikazi katika wilaya hiyo kuelekea katika kijiji hicho hata hivyo
msafara huo haukuweza kuvuka mto mkubwa wa Ilyamchele na magari
kutokana na kutokuwepo kwa daraja linalounganisha kijiji hicho ambapo
leo ndiyo limewekwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo
na Ndugu Abdulrahman Kinana.
Baada
ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo Kinana pamoja na
msafara wake walivuka mto huo kwenye daraja la miti lililotengenezwa kwa
nguvu za wananchi. kisha alipanda pikipiki na kuelekea katika mkutano
mdogo na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele ambacho kimo katika msitu wa
akiba kata ya Nyamonge wilayani Bukombe mkoani Geita.
Kinana
yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza
ambapo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Kagera sasa anaendelea na
ziara hiyo katika mkoa wa Geita kabla ya kumalizia ziara yake mkoani
Mwanza akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akivuka na wananchi katika daraja hilo.

Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mjini Bukombe,mkoani Geita

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubi Wananchi katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitema chehe katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiunguruma katika mkutano wa hadhara mjini Bukombe

Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu Kinana kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukombe,

Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu Kinana alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukombe.

Katibu
Mkuu Ndugu Kinana akishiriki kufitisha fremu ya mlango katika vyumba
vya madara ya Shule ya Sekondari ya Busonge, wilayani Bukombe, Mkoa wa
Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki kutega mzinga wa nyuki katika Kata ya Iyogelo, wilayani Bukombem Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe, Geita.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wakitafuta dhahabu wilayani Bukombe.

Ndugu
Kinana akizungumza na wajasiliamali wa uuzaji wa samaki na dagaa katika
Soko la Uyovu katika Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe.

Wananchi wa Kijiji cha Ilyamchele wakisindikiza kwa ngoma msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Nape Nnauye

Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Msingi ya Ilamchele, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.

Sehemu
ya chumba cha darasa cha Shulre ya Msingi Ilyamchele, katika Kata ya
Namonge, wilayani Bukombe. Ndugu Kinana baada ya kuona hali hiyo,
aliitisha harambee ya ujenzi wa shule hiyo, isiyokuwa na walimu
wataalamu

Ujenzi wa vyumba viwili vya darasa katika Shule ya Msingi ya Ilyamchele ukiendelea, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitumia usafiri wa pikipiki alipokuwa
anakwenda Kijiji cha Ilyamchele, Kata ya Namonge ambako aliendesha
harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ilyamchele akiwa katika ziara
wilayani Bukombe, Geita, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza
kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Wananchi wakivuka daraja la Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita

Wananchi wakivuka daraja la Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana akivunja muwa na baadhi ya watendaji wa
Halmashauri ya Bukombe wakati akirejea mara baada ya mkutano wake na
wananchi wa kijiji cha Ilyanchele.

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua muwa na baadhi ya watendaji wa
Halmashauri ya Bukombe wakati akirejea mara baada ya mkutano wake na
wananchi wa kijiji cha Ilyanchele.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizindua ujenzi wa wa dara la Ulyamchele,wilayani Bukombe mkoani Geita.

Gari
lililombeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye likivuka
katika moja ya mito katika Kijiji cha Ilyamchele, wilayani Bukombe.

Msafara wa Komredi Kinana ukivuka katika moja ya mio iliyopo Barabara ya Ilyamchele
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM Tawi la Busonzo, wilayani Bukombe
No comments:
Post a Comment