TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO DAR
Wanafunzi
wenye ulemavu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Abisina Rashid (kulia) na
Rozalia Polycarp (wa pili kulia), wakishiriki katika uzinduzi wa kisima
cha maji kwa kufungua maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kukabidhi msaada wa kisima hicho kwa shule hiyo Dar es Salaam jana.
Kisima hicho kitakachohudumia pia Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa
ujenzi wake ulisimamiwa na Kampuni ya Winners. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho,
Balozi mstaafu,Herman Mkwizu, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto),Ofisa
Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni na Mwalimu Mkuu wa
shule hiyo, Anna Mshana.
Ofisa
Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia)
akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Zarina Kigoma baada ya Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kwa Shule ya Uhuru
Mchanganyiko, Dar es Salaam jana.Anayeshangilia kushoto ni Mwalimu Mkuu
wa shule hiyo, Anna Mshana.Kisima hicho kitakuwa kinahudumia pia Shule
ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo
(kulia) akinywa maji ya bomba baada ya kukabidhi msaada wa kisima kwa
Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Ofisa
Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho.
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa kuona akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu kwao.
No comments:
Post a Comment