Watumishi Bodi ya Bodi ya Mikopo watakiwa kuongeza ufanisi

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) Bw. George Nyatega (mwenye tai) akipokea tuzo kutoka kwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi,
Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) - Tawi la HESLB Bw. Deodatus
Mwiliko kutambua uongozi wake bora katika HESLB tangu ilipoanzishwa
mwaka 2005. Wengine ni viongozi wa RAAWU-HESLB Bw. Luhano Lupogo na Bi.
Octavia Selemani. Picha: HESLB
Watumishi wa Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wametakiwa kuongeza ufanisi
katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuondokana na malalamiko kutoka kwa
wanafunzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega ametoa wito huo mara baada ya kukabidhiwa tuzo
na Chama cha Wafanyakazi
wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU),
tawi la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Akiongea
katika hafla fupi ya kukabidhi ngao hiyo, Mwenyekiti wa RAAWU Tawi la HESLB Bw.
Deodatus Mwiliko alisema RAAWU, Tawi la HESLB imeamua kumkabidhi Mkurugenzi
mtendaji huyo ngao hiyo kutokana na kujali na kuboresha mazingira ya kufanya
kazi kwa watumishi wote wa HESLB.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema amepokea
tuzo hiyo kwa niaba ya menejimenti anayoingoza na wafanyakazi wote na kuwataka
watumishi wa HESLB kutoridhika na ufanisi uliopo na badala yake waongeze
juhudi.
“Ninapokea
hii ngao kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wote kwa sababu sifanyi kazi
peke yangu,” alisema Bw. Nyatega leo (Alhamisi, Mei 28, 2015) katika makao
makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.
“Ninawapongeza
kwa kufanya kazi kwa ufanisi, lakini pia muongeze juhudi katika utoaji wa
huduma kwa wanafunzi ili pasiwe na malalamiko,” amesema Bw. Nyatega.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi
Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Tangu kuanzishwa kwake, Bw. Nyatega
amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake.
No comments:
Post a Comment