TAMWA Kuwajengea Uwezo Waandishi Uandishi Habari za Uchaguzi
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo akizungumza na baadhi
ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam
katika mkutano na wahariri hao.
Sehemu
ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano
ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na
kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano
ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na
kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha
Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kimepanga kuwajengea uwezo baadhi
ya waandishi wa habari nchini juu ya uandishi wa habari za uchaguzi
kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2015.
Akizungumza
katika mkutano na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi.
Gradness Munuo alisema mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi wanahabari juu
ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa ujumla kwa kuzingatia utoaji wa
nafasi kwa makundi ya wanawake,
vijana
na watu wenye ulemavu. Alisema kundi la wanawake wanaoshiriki kugombea
katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi na walemavu wamekuwa wakikosa
fursa kwenye vyombo vya habari kujinadi kutokana na mfumo na mazingira
ya uchaguzi yalivyo, hivyo kuna haja ya kuwajengea uwezo wanahabari ili
waweze kuzipa kipaumbele pia na makundi hayo ambayo huachwa nyuma kwenye
mchakato mzima.
No comments:
Post a Comment