ENG. STELLA MANYANYA AONANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA JIANGXI KUTOKA CHINA INAYOJENGA BARABARA YA LAMI MKOANI RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa Kampuni ya
Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China ikiongozwa na
Mtendaji Mkuu Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia ofisini kwake leo
tarehe22/05/2015. Kampuni hiyo inajenga barabara ya lami kuunganisha
Mkoa wa Rukwa na Katavi katika mradi wa Sumbawanga-Kanazi (KM 75). Mkuu
huyo wa Mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ushirikiano wake mzuri na
uongozi wa Mkoa katika shughuli zake za ujenzi wa barabara hiyo.

Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus
Rugarabamu akiongoza zoezi la utambulisho wa wageni na wenyeji katika
kikao hicho.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng.
Zhu Chunhua wa pili kulia akizungumza katika kikao hicho ambapo
ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano unaowapa katika
kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami ya Sumbawanga – Kanazi, aliongeza
kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya kazi zingine mbalimbali Mkoani
Rukwa ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka pamoja na
kuwekeza katika eneo la ufugaji.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng.
Zhu Chunhua akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella
Manyanya walipomtembelea Ofisini kwake leo. Barabara ya Lami ya
Sumbawanga – Kanazi – Namanyere – Kizi – Kibaoni inajengwa kwa fedha za
Serikali ya Tanzania na ujenzi wake bado unaendelea.

Picha ya pamoja.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua muda mfupi kabla ya kuagana mapema leo. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

No comments:
Post a Comment