MAMBA WANAOUA WATU KUDHIBITIWA-MASASI
Wanakijiji
wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu
waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta
machozi kutoka wizarani kwake.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa
Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine
kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani
kwake.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaagiza
askari na maofisa wa wanyamapori nchini kuwavuna mamba wanaoua na kujeruhi
wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Manyuli wilayani Masasi mkoani Mtwara, alipokwenda kukagua madhara
yatokanayo na mamba katika Mto Ruvuma.
Kauli ya Nyalandu imetokana na kilio cha Mbunge wa Masasi,
Mariam Masembe na wananchi wake kuwa mamba hao mbali na kuua na kujeruhi
wananchi, pia wamekuwa kero kubwa na kusababisha shughuli za uzalishaji mali
kuzorota.
No comments:
Post a Comment