Header Ads

TAMASHA LA QASWIDA SASA KUFANYIKA MEI 31 JIJINI DAR

 Pichani kati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre,Jumanne Ali Ligopora   akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam kuhusiana na tamasha la Qaswida,linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza.
 Mmoja wa watakaoshiriki katika tamasha hilo,Rahma Muhidin Kigora akighani Qaswida mbele ya waandishi wa habari  (hawapo pichani).
 Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo uliohusu 
tamasha la Qaswida,linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza. 

Tamasha la Qaswida lililokuwa likitarajiwa kufanyika Mei 25,jijini Dar,sasa limepangwa kufanyika Mei 31 katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo,kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre,Jumanne Ali Ligopora amesema kuwa tamasha hilo limebadili tarehe ya onesho lake ili kuwa bora zaidi.
Amesema kuwa tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake,tayari lmekwishawapata wadhamini watatu,amewataja wadhamini hao kuwa ni Gazeti la Dira ya Mtanzania, watengenezaji wa kinywaji cha Sayona na Madrasamtimun.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika mashindano hayo kutakuwepo na watu wa benki za miamala ya kiislam,ambao wataonesha namna benki hizo zinavyofanya kazi na huduma kwa wateja wao.

No comments:

Powered by Blogger.