SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),
George Mkuchika akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa uwazi na
kusikilizana kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali barani
Afrika mkutano uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO Issah Mwambene akichangia kwa upande wa
serikali kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu, wakati wa mkutano wa Uwazi
na usikivu katika mambo ya uchumi serikalini pamoja na taasisi zisizo
za kiserikali katika bara la Afrika.

Mkurugezi wa kampuni ya Compass
Communications Ltd Maria Sarungi akizungumza katika mkutano wa Uwazi
na Usikivu uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika,
mkutano hup umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugeni Mkuu wa TWAWEZA Aidani Eyakuza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika kufunga mkutano uliowakutanisha
wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya Wadau wa mkutano kutoka nchi mbalimbali za Barani Afrika walihudhuria mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUWA WAZI.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Serikali
na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali Barani Afrika zimetakiwa
kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya uendeshaji wa mambo yake
kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George
Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau
mbalimbali Barani Afrika kutoka serikalini na Taasisi zisizo za
kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu
Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.
Mkuchika
amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku
mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo
mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema
kufanikisha malengo ya nchi.
Pia
kwa upande wa serikali amesema kuwa serikali ikiweka mambo yake kwa
uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi
inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu
nini kinaendelea katika nchi husika.
No comments:
Post a Comment