ZIARA YA MAFUNZO YA UJUMBE WA SERIKALI YA ZIMBABWE NCHINI
Mwenyekiti
wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Dkt. Steven James Bwana
akiukaribisha ujumbe wa Serikali ya Zimbabwe katika Ofisi ya Tume ya
Utumishi wa Umma Tanzania ilipofanya ziara ya Mafunzo nchini Tanzania jana.

Katibu
Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Richard Odongo akiwasilisha
mada wakati wa Ziara ya Mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe
ilipoitembelea ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma nchini jana.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi
akiukaribisha Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo jana.
Baadhi
ya Maofisa wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa
Umma ya Zimbabwe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa
ulipoitembelea ofisi ya Rais-Utumishi.

Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi (wa pili kushoto) Bw. Francis Sangunaa
akiwasilisha mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo jana.
Mkuu
wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za
Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi. Sarah Kibonde akiwasilisha
mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe
ulipoitembelea ofisi hiyo jana.

Makamu
Mwenyekiti wa Tume Ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe Dkt. M. Muchada
akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi.
Sarah Kibonde mara baada ya baada ya kumaliza ziara ya mafunzo katika
ofisi hiyo jana jioni.
No comments:
Post a Comment