RAIS KIKWETE AKAGUA WAATHIRIKA WA MAFURIKO BUGURUNI
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko kutoka katika
nyumba
za watu katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya ya Ilala jijini Dar
es Salaam leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi
mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na
kuwafariji wananchi.

Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni
Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji
ya mafuriko wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi
mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na
kuwafariji wananchi.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao
imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.


Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha
mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es
Salaam leo.
No comments:
Post a Comment