ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA VUNJO MKOANI KILIMANJARO

Wananchi wa Kata ya
Makuyuni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye
aliwaambia kwa miaka mingi sasa jimbo la Vunjo limekuwa linarudishwa nyuma na
ushabiki wa kisiasa na kuwataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi mwaka huu
kwa kuichagua CCM.

katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisikiliza moja ya swali lililokuwa
likiulizwa na mmoja wakazi wa himo,Bi.Pepetua Shayo kuhusiana na mradi
wa maji uliopo katika eneo hilo,ambapo baadhi ya wananchi wamechukuliwa
maeneo yao bila kulipwa fidia yoyote.

Kijana kutoka chama cha
Chadema Membeck Kaigarula akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana na kutangaza rasmi kujiunga na CCM kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Himo.

Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye uwanja wa polisi Himo
ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya
msingi kwa kuchagua kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyiaka kwenye viwanja vya polisi himo na kuwaambia
wananchi hao wapinzani hawana tena ubavu wa kuongoza kwani kwa zaidi ya
miaka mingi sasa wamepata nafasi na hamna walichokifanya kwa wananchi
hao wa jimbo la Vunjo.

Naibu Kamanda wa UVCCM Moshi Vijijini,Innocent
Shirima akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh.Novatus
Makunga,kabala ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia wakazi wa Vunjo.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnaupe pichani kushoto na wajumbe wangine wakitembea kuelekea kwenye
uwaja wa mkutano wa hadhara,mjini himo.

Katibu
Mkuu wa CCM akinunua ndizi barabarani Himo wakati akielekea kwenye uwanja wa
mkutano wa hadhara

Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwenye mradi wa vijana wa
kijiji cha Oria ,kata ya Kahe Magharibi.
Baadhi ya wananchi
wakishangilia jambo kwenye uwanja wa polisi Himo ambapo aliwaambia wananchi hao
kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya msingi kwa kuchagua kiongozi
anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.

No comments:
Post a Comment