Mrithi wa Zitto PAC ziarani Afrika Kusini
Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini.
MWENYEKITI
mpya wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau,
ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara nchini ya Afrika
Kusini.
Wakiwa
nchini humo walitembelea Bandari ya Durban, ambapo walifanya mazungumzo
na viongozi wa juu wa bandari hiyo wakiongozwa na Meneja wake Vusi
Khumalo.
Mwidau
ambaye ameambatana na wajumbe kadhaa wa PAC akiwemo Makamu Mwenyekiti
Deo Filikunjombe, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage pamoja na
Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo.
.jpg)
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau akiwa
na Meneja wa Bandari Durban nchini Afrika Kusini, Vusi Khumalo wakati
kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi nchini humo, Machi 24 na 25 mwaka
huu.
.jpg)
Mwidau akiwa na wajumbe wa PAC, Ismail Rage pamoja na Gaudence Kayombo wakipata maelezo
No comments:
Post a Comment