Wananchi wa Vunjo wamchangia Innocent Melleck shirima kuchukua fomu ya ubunge vunjo
WANANCHI wa jimbo la Vunjo mkoani
Kilimanjaro wakiwamo wajasiliamali wadogo wamechangishana shilingi
milioni tisa na kumkabidhi Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM), Innocent Melleck kwa ajili ya kuchukulia fomu
ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mdogo wa himo baadhi ya wananchi hao Halid Msango,Jonas Mamuya na Aisha Mkwizu walisema kwa pamoja wananchi wa jimbo la Vunjo bila kujali itikadi zao za vyama wamemchangia kiasi hicho cha fedha ili kimsaidie kuchukulia fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda utakapofika.
Katika tukio hili tumeshiriki wananchi wa jimbo hili la Vunjo
kwa umoja wetu bila kujali itikadi za kisiasa ambapo hapa pia wapo
wanachama wa vyama vya NCCR Mageuzi,TLP,CHADEMA na CCM soote
tumeshiriki katika kuchanga fedha hizi lakini pia wapo makundi
mbalimbali kama vile mama lishe, madereva wa Bodaboda, wauza mboga, na
vijana wengine wanaofanya biashara ndogondogo na wapiga debe kwenye
vituo vya mabasi ya daladala.
Aidsha wananchi wao waliafikiana
kuunda kamati ya kuzunguka jimbo zima kuhakikisha kuwa wanakusanya fedha
za michango na kuhamasishana kwaajili ya kuhakikisha Melleck anapata
ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika kamati hiyo mwenyekiti ni
Mzee shayo na katibu wa mwika kuwa katibu huku katibu kata kata ya
kilema kusini Shabani Kwezi kuwa mjumbe na wajumbe wawili toka kila kata
za jimbo hilo hivyo kuwa na jumla ya wajumbe 36 katika kamati hiyo
ambayo ilianza majukumu yake mara moja.
Alisema zoezi hilo liliongozwa na zaidi ya wajumbe 1000 wa nyumba 10 wa CCM na kumtaka, Melleck kuchukua fomu ya kuwani nafasi hiyo ya uwakilishi katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Bwana Melleck aliwashukuru wananchi hao kwa
ujasiri mkubwa na Imani kubwa walioonyesha kwake , nimefarijika sana
kuona wananchi wenye kipato kidogo cha fedha wanachanga kiasi hiki cha
fedha na kunikabidhi ili nichukulie fomu na mimi naahidi kutowaangusha
kwa hilo, nitafanya hivyo muda ukifika,” alisema .
No comments:
Post a Comment