WAFANYAKAZI HOTELI YA SNOWCREST ARUSHA WALILIA MISHAHARA YAO

Baadhi
ya watumishi katika hoteli yenye hadhi ya nyota nne ya Snowcrest Hotel
ya jijini Arusha wameushutumu uongozi wa hoteli hiyo kwa kushindwa
kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Januari hadi sasa.
Pia
wameiangukia serikali kwa kuitaka iingilie kati suala hilo kwa kuwa
pamoja na kuwasilisha madai yao katika idara mbalimbali za serikali
mkoani hapa lakini hadi sasa wameshindwa kupatiwa ufumbuzi wa madai yao.
Hoteli
hiyo ni ile ambayo ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009 na
kisha kuvunjwa ghafla na Wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads)
baada ya ukuta wake kudaiwa kujengwa katika eneo la hifadhi ya barabara
ya Arusha-Moshi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti watumishi hao kwa sharti la kutotajwa majina yao
hadharani kwa sababu za kiusalama walidai kuwa uongozi wa hoteli hiyo
umeshindwa kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Januari hadi sasa.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti na gazeti hili walidai kuwa kitendo cha wao
kutolipwa mishahara yao kimechangia ukali wa maisha kwa kuwa baadhi yao
wameshindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni na hata kushindwa kumudu
kulipia kodi za nyumba zao.
No comments:
Post a Comment