CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTILIANA SAINI YA MKATABA WA MAKUBALIANO YA MAFUNZO YA WATALAAM WA TAKWIMU NA CHUO CHA TAKWIMU CHA INDIA.
Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya kutiliana saini ya
mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu
cha nchini India.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent
Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
“Maandalizi ya
kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo
cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa
mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa
ajili ya kujirizisha”, amesema Prof. Ngalinda.
Prof. Ngalinda amesema
kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam
wengi katika tasnia ya takwimu hapa nchini.
Pamoja na ongezeko la
watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na ukarabati wa miundombinu katika
chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
No comments:
Post a Comment