PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA MAKAO MAKUU:KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AVISHA YEO MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja
akikagua Gadi Maalum ya Heshima iliyoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la
Magereza katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa waliopandishwa vyeo
ngazi mbalimbali(jana) Machi 20, 2015 katika Viwanja vya Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.

Bendi ya Jeshi la Magereza ikipita mbele ya Mgeni rasmi Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) kutoa heshima
baada ya zoezi la uvishaji vyeo Maafisa 77 wa vyeo mbalimbali
kukamilika.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza(CGP), John Casmir Minja akimvisha
cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa
waliopandishwa vyeo ngazi mbalimbali(jana) Machi 20, 2015 katika Viwanja
ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment