Header Ads

Kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni

Picha juu na chini ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Bingwa, Dimba na Mtanzania kutoka Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Sharifa Mmasi pichani akisoma kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichoandikwa na Kambi Mbwana, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka wilayani Handeni, mkoani Tanga. 

MWANDISHI wa Habari za Michezo ambaye pia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, ameandika kitabu chake kinachojulikana kama ‘Dira na Tumaini Jipya Handeni’, kilichoanza kupatikana mapema wiki hii jijini Dar es Salaam na wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Kitabu hicho kimeelezea kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa Handeni, kama vile shida ya maji, elimu na migogoro ya ardhi kwa ajili ya kushirikisha mawazo ya viongozi wa serikali, wadau na wananchi ili kukabiliana na tatizo hilo wilayani humo na mikoa ya jirani ambapo changamoto hizo zinashabihiana kwa kiasi kikubwa.
Sharifa Mmasi akisoma kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni, kilichoandikwa na Kambi Mbwana.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mbwana alisema kwamba kuandika kitabu hicho kuna lengo kubwa la kuelimisha jamii kwa ajili ya kutafuta fursa ya kimaendeleo katika wakati huu ambao wananchi wengi wamekuwa wakilia bila kupata msaada wowote.

“Naijua vizuri wilaya yangu ya Handeni na mkoa wa Tanga kwa ujumla, hivyo nimeamua nitumie kipaji change katika kuandika kitabu hiki ambacho kimeweza kuanika mambo mengi yenye tija kwa serikali na wananchi kwa ujumla, hivyo naomba waniunge mkono kwa kuhakikisha kwamba wanapata kitabu hiki popote kitakapokuwapo.

No comments:

Powered by Blogger.