ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA MBEYA MJINI NA MBEYA VIJIJINI


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Kimondo, Mbeya Vijijini kabla ya
kuweka jiwe la Msingi la zahanati yao akiwa katika ziara ya mkoa wa
Mbeya Februari 25, 2015. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbeya Vijijini,
Luckson Mwanjale na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman
Sigalla.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akikagua soko Kuu la Mjini Mbeya la Mwanjelwa baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25,
2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akiwasikiliza wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwambe
mjini Mbeya
wakati alipofungua na kukagua maabara tatu za shule hiyo akiwa katika
ziara ya mkoa wa Mbeaya Februari 25, 2015. Kushoto ni mkewe Tunu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na wananchi baada ya kufungua vyumba vitatu vya Maabara
katika shule ya sekondari ya Songwe mkoani Mbeya Febrari 25, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Max Oswald (kushoto) na Ivan Kina
wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda katika kijiji cha Igoma , Mbeya Vijijini Februari 25,
2015.
.

Wasanii Max Oswald ( Wapili Kulia)
na Ivan Kina (wapili kushoto) wakisaidiwa kuvua nyasi walizokuwa
wamejifunika kwa ajili ya kutoa burudani katika mkutano wa hadhara
uliohutuibiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katia kijiji cha Igoma,
Mbeya vijijini Februari 25, 2015. Wanaowasaidia ni Oscar Ben (kulia) na
Obadia Dandu.
No comments:
Post a Comment