Header Ads

Picha Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Tazama Matukio Mbalimbali ya Ziara ya Kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe nchini Uturuki

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akisalimiana na Naibu Meya wa jiji la Ankara ambaye naye alikuja Uwanja wa Ndege kumlaki
Waziri Membe kushoto akibadilishana mawazo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania katika Chumba cha Wageni Maalum kwenye Uwanja wa Ndege wa Ankara
 Naibu Meya wa jiji la Ankara aliyeketi kushoto akibadilishana mawazo na Mhe. Membe kabala ya kuondoka kutoka katika kiwanja hicho
 Waziri Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anawakilisha Uturuki aliyekaa kushoto pamoja na Bw. Salvator Mbilinyi, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia aliyechutama wakibadilishana machache katika Chumba cha Wageni Maalum ndani ya Uwanja wa Ndege wa Ankara.
 Waziri Membe akiendelea kuwahutubia waandishi wa habari hawapo pichani
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe akihutubia Mkutano wa Waandishi wa Habari huku akimshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Almet Dovutoglu
 
Waziri Membe kulia akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Uturuki mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo.
 Waziri Mkuu wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Ankara, Uturuki tarehe 08 Mei, 2014.

No comments:

Powered by Blogger.