Muungano wa Tanzania ni kielelezo cha maendeleo.
![]() |
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan leo mjini Dodoma.
(PICHA NA HASSAN SILAYO)
|
Na Jovina Bujulu
Muungano wa Tanzania umeendelea kuwa nyenzo na utambulisho muhimu katika kuleta umoja na maendeleo katika taifa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mh.
Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini
Dodoma.
“Miaka
50 ya Muungano imekuwa ni ya mafanikio makubwa ambayo yamewanufaisha
wananchi katika nyaja mbalimbali kijamii, kiuchumi, na Kisiasa” alisema
Waziri Suluhu.
Waziri
Samia alisema kuwa muungano huo umeendelea kuwa kielelezo imara katika
suala la ulinzi na usalama hali iliyowezesha kuwepo kwa amani na utulivu
nchini.
Katika
suala la haki za binadamu Waziri Samia alisema kuwa suala hilo
limeendelea kupewa kipaumbele ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambapo wananchi wameendelea kupata haki zao za msingi kupitia
mahakama za Mwanzo hadi za Juu.
Akifafanua
kuhusu suala la elimu Waziri Samia alibainisha kuwa wanafunzi wenye
sifa Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa mikopo ili kukidhi gharama za
Masomo, hali iliyosabisha uimarishwaji wa elimu ya juu kwani kuwekuwepo
kwa ongezeko la vyuo vya elimu ya juu kutoka 25 mwaka 2015 hadi 63
vilivyopo sasa.
Aidha
Waziri Samia alisema kuwa Serikali hizi mbili zinashirikiana katika
kubuni na kuibua miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Serikali kwa
Kushirikiana na Wahisanai wa Maendeleo.
“Serikali
hizi zimekuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya mandeleo mfano
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF III, MACEMP, ASDPL na ASDP kwa ujumla
imekuwa ni chachu kubwa ya Maendeleo ya wananchi katika pande zote za
Muungano” Alisema Waziri Samia.
Waziri
Samia aliongeza kuwa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa
Zanzibar tarehe 1 Machi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein
ambapo nembo ya Muungano ilizinduliwa na sherehe za Muungano zitafanyika
Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Utanzania wetu ni Muungano wetu, Tuulinde, Tuumarishe na Kuudumisha.”
Doreen Noni kushiriki shindano la Africa Magic Choice Awards Lagos
Mjasiriamali
na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Doreen Noni akizungumza kwenye
Exclusive Interview na mtandao wa habari wa MOblog.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MJASIRIAMALI
na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Doreen Noni anatarajiwa kushiriki
kwenye shindano la kumtafuta mbunifu bora katika sanaa ya filamu,
(Africa Magic Viewers Choice Awards) nchini Nigeria wiki hii.
Akizungumza
na MOblog Tanzania, hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Noni amesema
kwamba amechaguliwa kushiriki katika shindano hilo la Africa Magic
Viewers Choice Awards baada ya kushiriki filamu ya siri ya mtungi. “Africa
magic viewer’s choice awards ni kama Oscar ya Afrika ambapo sinema zote
wanazotizama watu kwenye Mnet, series na nia hasa ni kutizama kazi za
wasanii mbali katika fani ya uingizaji wa filamu Afrika,” amesema.
Amesema
alifanikiwa kufanya kazi na kampuni ya (Media for Development
International) ambao wanafanya kazi ya kuhamasisha kazi za uzalishaji
katika filamu za Afrika ili kutambua mchango wa wasanii mbalimbali
katika bara hili.
Noni
amesema kuwa kupitia kampuni au shirika hilo lisilo kuwa la kiserikali
aliweza kushiriki kwenye filamu ya “Siri ya Mtungi” ambapo alitengeneza
nguo na mavazi yote yaliyotumika katika filamu hiyo.
Amesema
kwamba katika filamu hiyo alitengeneza nguo kwa kila mshiriki wa filamu
baada ya kuzunguka katika masoko mengi ya jijini Dar es Salaam katika
kutafuta nguo zinazoendana. “nimechaguliwa
baaada ya kupeleka baadhi ya kazi zangu za kisanii hasa kwa design na
kubuni mavazi mbalimbali baada ya kuonyesha kipaji chake katika
tamthilia hiyo ya Siri ya Mtungi,” alilisitiza.
Noni
amesema kwamba yeye ana malengo yake kama kijana na mjasirimali ni
kufika mbali katika fani yake hiyo ya ubunifu wa mavazi na
ujasiriamali. MJASIRIAMALI na mbunifu
wa mavazi anayekuja juu nchini Tanzania, Doreen Noni anatarajiwa
kushiriki kwenye shindano la kumtafuta mbunifu bora katika sanaa ya
filamu, Africa Magic Choice Awards nchini Nigeria.


No comments:
Post a Comment