MANGULA AISIMANGA CHADEMA KALENGA, ASEMA CCM LAZIMA ISHINDE
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi wa
CCM katika kata ya Mgama kijiji cha Mgama mara baada ya kuwasili kjijini
hapo kwa ajili ya kufanya mkutano na wajumbe wa harmashauri kuu ya Kata
hiyo ili kujadili kwa pamoja mwennendo wa kampeni katika jimbo la
Kalenga ambapo chama hicho kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa kuwa
mgombea wa jimbo hilo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka
huu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kuimba wimbo na
wana CCM mara baada ya kuwasili katika kikao hicho cha ndani
kilichofanyika kwenye kijiji cha Mgama.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kucheza ngoma
kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa ndani uliofanyika leo kwenye kijiji
Mgama
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifurahia jambo kwa kupiga
makofi wakati wa mkutano huo wa ndani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Iringa
Vijijini mama Delfina Mtavilalu.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza na waandishi wa
habari kijijini Mgama mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisoma mambo muhimu yanayohusu uchaguzi huo kwa wana CCM.
Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula ukiwasili katika kijiji cha Mgama
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisisitiza jambo wakati
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
wa ndani
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisisitiza jambo wakati
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
wa ndani
................................................................................................
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama
cha CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa
kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.
Mangula amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda
uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini.
Kiongozi huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha
Mugama kata ya Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa
halmashauri kuu ya CCM ya kata hiyo.
Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM
kata ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho
ni mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda.
Samson alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya
Mugama jambo linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu
chafu
ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake.
Baada ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo
ndani ya kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na
wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika.
“CHADEMA hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza
kusema kina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au
wanataka
kuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema.
Alisema CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na
mafanikio na utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo
mambo
mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa.
Kwa mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa
CCM hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe
ahadi zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi,
alisema Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo
hakuna
mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo.
Betha alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi
yote yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi
wake
siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura.
Alisema viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele
kuhamasisha amani kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili
kuhakikisha
ubnafanyika kwa amani.
Aidha, alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu
wa aina yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na
jimbo la Kalenga kwa jumla.
Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa
kufanyika Machi 16, mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa
kuwa mgombea wake atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo
unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa
kufariki dunia Januari mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini
Afrika Kusini.

No comments:
Post a Comment