Wajumbe wa Bodi Wavutiwa na Teknolojia ya Utengenezaji Kadi ya Mwanachama NSSF
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (mwenye
kofia nyeupe) akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF, Ester Msalahi,
ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi ya binafsi. Kadi hilo
iliandaliwa ndani ya saa moja kwa teknolojia mpya ya kisasa 'Mobile POS'
ya utengenezaji kadi ya mwanachama wa shirika hilo
Wajumbe wa Bodi ya NSSF pamoja na viongozi wa shirika hilo wakipata maelezo juu ya Mobile POS inavyofanya kazi.
Mmoja wa wafanyakazi wa NSSF tawi la Ilala (katikati) aliyezungukwa
akitoa maelezo namna Mobile POS inavyorahisisha kazi ya utengenezaji
kadi ya mwanachama wa NSSF kwa muda mfupi.
Meneja Kiongozi wa NSSF Temeke, Yahaya Mhamali (kulia) akitoa ufafanuzi
juu ya teknolojia mpya ya kutoa huduma zote kwa wateja wao kwa kutumia
tiketi maalumu ambayo mteja huchukua kwenye mashine maalumu anapofika
kupata huduma anuai.

Wajumbe wa Bodi ya NSSF pamoja na viongozi wa shirika hilo wakipata
maelezo namna teknolojia mpya ya kuhudumia wateja inavyofanya kazi eneo
hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (kulia)
akimnong'oneza jambo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau
walipokuwa katika ziara ya wajumbe wa modi katika moja ya miradi
inayotekelezwa na shirika hilo
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akitoa ufafanuzi juu ya jengo jipya la NSSF lililopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa NSSF pamoja na wahandisi wa jengo hilo
wakiangalia maendeleo wa jengo jipya la NSSF lililopo Ilala Jijini Dar
es Salaam

Muonekano wa jengo hilo likiwa katika hatua za mwisho.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa NSSF pamoja na wahandisi wa jengo hilo
wakiangalia maendeleo ya jengo jipya la NSSF lililopo Ilala Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa NSSF pamoja na wahandisi wa jengo hilo
wakiangalia maendeleo ya jengo jipya la NSSF lililopo Ilala Jijini Dar
es Salaam.
WAJUMBE
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
jana jijini Dar es Salaam walivutiwa na teknolojia mpya inayotumiwa kwa
sasa na Shirika hilo katika utengenezaji wa kadi ya mwanachama wa NSSF.
Teknolojia hiyo mpya (mobile POS) ya utengenezaji wa kadi ya mwanachama
wa NSSF imerahisisha maradufu muda wa awali wa utengenezaji wa kadi ya
mwanachama (smart card) kutoka takribani wiki moja hadi ndani ya saa
moja kwa sasa.
Wakitembelea
miradi mbalimbali ya NSSF jana jijini Dar es Salaam Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NSSF walishuhudia teknolojia hiyo katika Tawi la NSSF
Temeke, ambapo walishuhudia wateja wakihudumiwa na kupata kadi ya
uanachama wa taasisi hiyo ndani ya saa moja tofauti na ilivyokuwa awali.
Akiwaelezea
Wajumbe wa Bodi, Meneja Kiongozi wa NSSF Temeke, Yahaya Mhamali, ambapo
teknolojia hiyo inatumika tangu mwishoni mwa mwaka jana, alisema
imeboresha shughuli za huduma kwa wateja kwani kwa sasa mteja anapata
kadi ya uwanachama ndani ya saa moja tofauti na awali ambapo ilichukua
takribani wiki moja kabla ya mteja kupata kadi hiyo.
Alisema
teknolojia ya ‘Mobile POS’ kwa sasa inawawezesha NSSF kwenda moja kwa
moja na kifaa hicho ofisi walipo wateja wao na kuingiza taarifa za
mtena, kuzihakiki na hata kutoa kadi ya mwanachama huyo kwa muda mfupi
tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema
kwa wateja wanaokuja wenyewe ofisini na kuwa na taarifa zao
hutengenezewa kadi ya uanachama ndani ya saa moja jambo ambalo
limeongeza ufanisi kihuduma tofauti na ilivyo kuwa hapo awali. “…Sasa
hivi mteja akija mwenyewe ofisini akiwa na taarifa zake sahihi anapata
kadi yake ndani ya saa moja na kuondoka,” alisema Mhamali.
Wajumbe
hao walishuhudia mmoja wa wateja aliyetambulika kwa jina la Ester
Msalahi, ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi ya binafsi
akihudumiwa na kupatiwa kadi yake ya uanachama ndani ya saa moja, ambapo
kadi hiyo ilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF,
Abubakar Rajabu huku akishughudiwa na wajumbe wa bodi na viongozi
waandamizi ya shirika hilo katika ziara hiyo.
NSSF
kwa sasa inatumia mfumo wa kompyuta wa kuwahudumia wateja katika ofisi
hiyo ambapo mteja uchukuwa tiketi ya huduma katika mashine maalumu
ambapo itampa maelekezo eneo analopaswa kuhudumiwa kwa wakati na kufuata
utaratibu.
Aidha
viongozi waandamizi wa NSSF walitembelea jengo jipya la NSSF
linalojengwa eneo la Ilala ambalo litakuwa na ghorofa 20 kwenda juu huku
likiwa na eneo la kuegesha magari la ghorofa nne ardhini. Ghorofa hilo
linalojengwa kisasa ambalo litakuwa likitumiwa na NSSF Mkoa wa Ilala pia
litakuwa na ofisi za kukodi, kumbi za mikutano benki na huduma zingine
za kawaida za jamii mjini.
Akifafanua
kwa wanahabari kuhusiana na ujenzi wa jengo hilo, Meneja Miradi wa
NSSF, Mhandisi John Msemo alisema jingo hilo kwa sasa limefikia hatua za
mwisho kukamilika kwani mafundi wanafanya matengenezo ya mwisho ili
kumalizia ujenzi huo.
“…Jengo
hili lipo katika hatua za mwisho kukamilika, sehemu kuwa ya ujenzi
imemalizika na kinachofanyika sasa ni kuweka miundombinu kama ya maji,
umeme na vutu vingine kama hivyo. Ghorofa hili pia kutakuwa na maeneo ya
kupangisha wateja kwa shughuli mbalimbali…,” alisema Msemo.
Akifafanua
zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa ghorofa hilo la kisasa
umegharimu shilingi za Kitanzania bilioni 40. Imeandaliwa na
www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment